Back to top

Miundombinu ya makaburi ajali ya MV Bukoba iboreshwe.

21 May 2020
Share

Wakati leo ikiwa ni kumbukizi ya miaka 24 ya ajali ya meli ya MV. Bukoba iliyotokea mei 21 mwaka 1996 katika Ziwa Victoria baadhi ya ndugu wa marehemu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo wameziomba mamlaka zinazohusika na utunzaji wa makaburi ya pamoja yaliyopo katika eneo la Igoma jijini Mwanza kukarabati miundombinu ya makaburi hayo.

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba, anasema mipango ya kujenga ukuta huo wa makaburi ya pamoja ya baadhi ya waliokufa maji kwenye ajali ya meli ya MV. Bukoba yaliyopo eneo la Igoma yanategemea mkandarasi atakapokamilisha kazi ya ujenzi wa mtaro.

Kumbukizi ya miaka 24 ya ajali ya meli ya MV. Bukoba iliyopinduka na kuzama mei 21 mwaka 1996 jirani na kisiwa cha Juma wakati ikikaribia kufika bandari ya Mwanza kaskazini, imehudhuriwa na waombolezaji wachache sana tofauti na miaka mingine.