Back to top

Mpango kuwashushia rungu waliotafuna milioni mia nne Buhingwe.

01 July 2020
Share

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango ameagiza kufanyika uchunguzi wa kina wa matumizi ya zaidi ya shilingi milioni mia nne  zilizotumika kujenga Kituo cha Afya Munzeze, wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, baada ya kutoridhishwa na ubora wa majengo ya kituo hicho.

Dkt.Mpango ametoa agizo hilo wakati akikagua ujenzi wa kituo hicho cha Afya ambacho kikikamilika kinatarajiwa kutoa huduma kwa zaidi ya wakazi elfu ishirini na tano wa kata hiyo, wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayopatiwa fedha na serikali.

Amesema uchunguzi huo ukibaini ubadhirifu, hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wote waliohusika na kuonya kuwa huu siyo wakati wa  kubembelezana.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina amesema atayafanyia kazi maelekezo ya Waziri wa Fedha na Mipango, kwa kuwa tayari alifanya ufuatiliaji wa mara kwa mara wa ujenzi wa kituo hicho.