
Rais wa chama cha Wanasheria wa Tanganyika na Mbunge wa Singida Mashariki Mh.Tundu Lisu amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu.
Tundu Lisu amekuwa akishikiliwa na polisi tangu Alhamisi ya wiki iliyopita baada ya kukamatwa uwanja wa wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere akituhumiwa kutoa lugha ya uchochezi.
Mapema asubuhi baadhi ya wafuasi wa Chadema na viongozi wao wamejitokeza makao makuu ya polisi kanda ya Dar es Salam kutaka kujua hatma yake huku wengine wakisambaratishwa.
Tundu Lisu anafikishwa Mahakamani muda mfupi baada ya wakili wake Fatma Karume kusema ombi lake kwa mteja wake kufikishwa Mahakamani limekubaliwa Mahakama kuu .