Back to top

NMB yaipa kongele IPP kwenye uwekezaji sekta ya habari nchini.

27 February 2020
Share

Uongozi wa Benki ya NMB umepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na makampuni ya IPP katika sekta ya habari hapa nchini.

Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kutembelea ITV, Redio One, Capital Tv ,Capital Redio  na East Afrika Tv na Redio kujionea shughuli za uendeshaji wa vituo hivyo, Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara Bwana Filbert Mponzi amesema amejionea uwekezaji mkubwa na kuvipongeza vituo vya IPP kwa kuwa vikongwe katika tasnia ya habari na program mbalimbali zikiwemo za vijana na wazee.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi na Afisa wa Bima wa benki hiyo Bwana Martine Massawe amesema kutokana na umuhimu wa bima benki hiyo imeanzisha huduma ya Bima kwa makundi mbalimbali wakiwemo wajasiliamali ili kujenga utamaduni wa kukata bima kwa ajili ya usalama wa  biashara na mali zao.