Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme amekataa kukabidhi madawati na meza katika shule ya msingi Mtakanini baada ya kubainika zimetengenezwa chini ya kiwango na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kuzifanyia marekebisho samani hizo.
Fedha za kutengeneza vifaa hivyo vilivyokataliwa kukabidhiwa na Bi.Mndeme zimetolewa na mfadhili Ramia Yasin ili kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati na meza katika shule hiyo lakini kwa uzembe wa halmashauri ya Namtumbo imetengenezwa samani hizo chini ya kiwango jambo ambalo halikubaiki.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mtakanini Bwana.Dahari Nilongo amesema samani hizo zimejengwa chini ya kiwango kutokana na kamati ya ujenzi ya shule ya msingi Mtakanini na uongozi wa kijiji kutoshirikishwa na halmashauri.