
Mmiliki wa timu ya soka ya Chelsea FC ya England Roman Abramovich ametangaza kuiuza timu hiyo ambapo amesema kuwa anafanya hivyo kwa maslahi mapana ya Timu, Wadhamini na Wafanyakazi huku akisisitiza kuwa siku zote amekuwa akifanya maamuzi kwa maslahi ya timu na kwa hali inavyoendelea sasa ameamua kuiuza timu hiyo
.
Roman Abramovich aliinunua timu hiyo mwaka 2003 kwa paundi milioni 140 sawa na Bilioni Tsh. 433/= ambapo kwa mujibu wa Jarida Forbes timu hiyo kwa sasa ina thamani ya paundi Bilioni 2.4 sawa na Trilioni Tsh. 7.4/= na ameamua kuiuza baada ya Urusi kuivamia Ukraine kuisababisha nchi hiyo na wawekezaji wake kuwekewa vikwazo au biashara zao kusitishwa sehemu mbalimbali ulimwenguni.