Back to top

SERIKALI YAGOMA KUONGEZA FEDHA UJENZI WA VETA

03 January 2023
Share

Serikali imekataa kuongeza fedha za ziada za gharama ya ukamilishaji wa miradi ya ujenzi wa Vyuo 10 vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), baada ya kubaini baadhi ya wataalamu wamekadiria matumizi ya fedha nyingi za umaliziaji wa miradi hiyo tofauti na gharama halisi.
.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Omary Kipanga wakati akikagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha VETA Mafia, ambao umegharimu zaidi ya Bil. 2, lakini fedha hazikutosha.