Back to top

Sipo tayari kuona rasilimali za Tanzania zikinufaisha nchi nyingine.

30 July 2018
Share

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayupo tayari kuona rasilimali za Tanzania zikinufaisha nchi nyingine na kuwa ni lazima kila upande unufaike na jinsi ulivyoshiriki katika uzalishaji wa rasilimali husika ama kuiongezea thamani.

Rais Magufuli amesema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akikabidhi hati za viwanja vya makazi na ofisi kwa balozi  mbalimbali na taasisi za kimataifa na kuongeza kuwa atahakikisha anaendelea kuwa kinara wa kupambania haki za watanzania.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Wilium Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge wamesema viwanja hivyo vimegharamiwa na serikali ya Tanzania na kuwa jukumu la balozi ama taasisi husika kuanza ujenzi na serikali itaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano kwao kufanikisha hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema pamoja na balozi na taasisi hizo za kimataifa kupewa hati hizo za umikili wa viwanja wanapaswa kuwasiliana na nchi zao kwa ajili ya ukamilishaji wa taratibu za kisheria za kuhusiana na umiliki wa maeneo hayo.