Back to top

TANZANIA YAPONGEZWA UWAZI VIRUSI VYA MARBURG

23 March 2023
Share

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt.Michael Battle, ameipongeza Tanzania kwa uwazi na utoaji wa haraka wa Taarifa kwa umma kuhusiana na ugonjwa wa Marburg ulioibuka mkoani Kagera.
.
Dkt.Battle ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu, kwenye ofisi za wizara hiyo zilizopo Jijini Dodoma.

.

"Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa wa wazi hasa katika utoaji wa taarifa za magonjwa ya mlipuko kwa haraka ikiwemo hii ya ugonjwa wa Murburg". Hakika mmeonyesha uongozi bora kwa dunia kuhusu usalama wa Afya kwa watanzania na dunia". Alisema Balozi Battle.