Back to top

Tozo ya Ving'amuzi yapunguzwa

27 June 2022
Share

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo amesema Serikali imepunguza tozo ya ving’amuzi nchini kutoka Tsh.1,000/= hadi Tsh.3,000/= iliyokuwa imependekezwa katika makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya serikali 2022/23 na kufikia Tsh.500/= hadi Tsh.2,000/= kadri ya matumizi ya mteja.
.
Sillo ameyasema hayo wakati akiwasilisha maoni ya kamati yake kuhusiana na Muswada wa Sheria ya Fedha 2022, bungeni jijini Dodoma.