
Amesema Ufaransa inatoa msaada katika mapambano dhidi ya ugaidi, kutokana na mahitaji ya nchi za kanda hiyo, sasa mamlaka ya Niger haitaki tena kupambana na ugaidi, hivyo itasimamisha ushirikiano huo wa kijeshi.
Ufaransa imesema itajadiliana na maofisa wa jeshi waliofanya mapinduzi nchini Niger, kuhusu mambo ya kuondoa jeshi kutoka nchi hiyo na inataka kazi hiyo ifanyike kwa utulivu.
Aidha, amesema balozi wa Ufaransa nchini Niger, atarejeshwa nyumbani ndani ya saa kadhaa.
Uamuzi huo wa Ufaransa umefuatia miezi kadhaa ya chuki na maandamano dhidi ya uwepo wa Wafaransa nchini humo, na maandamano ya mara kwa mara katika mji mkuu wa Niamey.