Back to top

WATOTO 32 WALA MATUNDA YENYE SUMU.

15 February 2023
Share

Watoto 32 wa darasa la awali wa miaka 5-6, wa  Shule ya Msingi Mkomo, iliyopo kata ya Chawi, Halmashauri ya mji Nanyamba, wanadaiwa kula matunda yenye sumu kutoka kwenye mti. 

Akizungumza shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mkomo, Bakari Likuani, amesema kuwa tukio hilo lilizua taharuki shuleni hapo, kwani Baada kula matunda hayo, mtoto mmoja alianza kutapika mwalimu alihisi anaumwa akamruhusu arudi nyumbani lakini baadae alikuta darasa zima linatapika.

Naye mmoja wa wakazi wa kijiji cha Mkomo amesema "Tulipofika na kuwakuta wanatapika sana alafu wamelegea tulionyeshwa mti huo hatua ya kwanza tuliukata na kuuondoa Kabisa katika eneo na hii itakuwa kampeni kwetu kila tunapoukuta tunauondoa kwa kuwa umeshakuwa adui wa watoto wetu”.

kwa upande wake Mganga Mfawidhi Msaidizi wa Zahanati ya Chawi, Kandidusi Fussi, amesema kuwa alipokea watoto 32 wenye umri kati ya miaka 5-6 wa darasa la awali, kutoka Shule ya Msingi Mkomo ambao waliofika wakiwa wanatapika na walikuwa wamelegea.