Wizara ya Maliasili na Utalii,imesema itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kutekeleza programu ya hifadhi na mifumo ikolojia inayovuka mipaka ya nchi kwenye nchi mbili au Zaidi, ili kuongeza nguvu katika udhibiti ujangili wa maliasili na kuimarisha ulinzi wa rasimali hizo kwa maslahi mapana ya taifa na Afrika kwa ujumla