Katika hotuba yake kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Bomas, Bwana Chebukati amesema zoezi la upigaji kura lilimalizika vyema katika vituo vingi na kwamba vituo 26,881 kati ya 46,229 kote nchini vimemaliza kuhesabu kura na kutuma fomu zake hadi Bomas.
Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 16 , vilivyotokea katika ajali ya gari Agosti 08, 2022 , katika Kata ya Mwakata, wilayani Kahama.
Mhe. Ndaki ameyasema hayo wakati wa hotuba yake ya Ufunguzi wa maonesho ya Nanenane kanda ya kati yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa baada ya Serikali kubaini changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi kama miongoni mwa sababu zilizoshusha ukuaji wa uchumi wa sekta hiyo.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Mashimba Ndaki ametumia jukwaa la ufunguzi wa maonesho ya Nanenane kanda ya Pwani Mashariki uliofanyika, mkoani Morogoro kuweka wazi mabadiliko ya teknolojia ambayo yamefanywa na Wizara yake kupitia sekta za Mifugo na Uvuvi.
Mfugaji kutoka Tengeru, Mkoani Arusha, Bw. Ayoub Urio amesema kuwa kituo cha NAIC kina mbegu bora za madume ya Ng'ombe na hivyo aliwahimiza wafugaji wengine ambao bado wanahimilisha mifugo yao kwa njia ya asili waache kufanya hivyo na watumie mbegu za NAIC.
Batista Ngwale mwenye umri wa miaka 27 amehukumiwa kifungo cha miaka 30 na Mahakama ya Wilaya ya Iringa baada ya kukutwa na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha nne...
Licha ya vitisho kutoka Beijing,nchini China Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, amewasili Taiwan na kuzungumza na Rais na Naibu Spika wa bunge, huku China ikifanya mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa hicho.