Watu saba wamefariki na wengine 21 kujeruhiwa ,baada ya gari la mashindano kuwaparamia watazamaji katika mashindano ya magari Fox Hill Supercross, siku ya Jumapili huko Diyatalawa, nchini Sri Lanka.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema viongozi na Watanzania wanajifunza mengi kutokana na historia ya utendaji kazi wa Mzee John Samwel Malecela, katika nyadhifa mbalimbali alizoshika Serikalini na Chama cha Mapinduzi na ataendelea kuwa hazina muhimu ya maarifa na uzalendo hapa nchini.
Amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha inaweka mazingira rafiki na wezeshi ya ushindani wa haki katika biashara na utoaji huduma , na kuzitaka mamlaka za udhibiti kutekeleza azma hiyo ya serikali.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mhe.Mama Mariam Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kutambua na kuthamini mchango wa Wanawake na kuwashirikisha katika ngazi ya maamuzi na kuendeleza maendeleo nchini.
Serikali za Tanzania na Zambia zimefanikiwa kufuta kero nne kati ya kero 15 zilizokuwepo awali ili kurahisisha michakato ya biashara ya nchi hizo kutegemeana kibiashara........