Back to top

WANANCHI FUATENI MAELEKEZO YA WATAALAM WA AFYA

19 March 2023
Share

Wananchi wa Mkoa wa Kagera wametakiwa kufuata maelekezo ya Wataalamu wa afya katika maeneo yao, ili kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya mlipuko.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel,amesema  serikali imejipanga kuhakikisha upatikanaji wa pesa, vifaa, dawa na rasilimali watu , ili kuhakikisha hali ya afya katika Mkoa wa Kagera inaimarika na utoaji huduma unakuwa bora.

"Tuendelee kuwaasa wananchi maelekezo yote ambayo Wataalamu wa afya wanayatoa mfano mambo ya kuzikana, hata kama mgonjwa hajaonesha dalili zinazofanana kama suala la maziko wayazingatie kwa Wataalamu na maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya"amesema Dkt.Mollel

Dkt.Mollel ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa namna walivojitoa katika kupambana dhidi ya magonjwa mbalimbali tangu kuibuka kwa ugonjwa usiojulikana Machi 16, 2023 Mkoani hapo.