Back to top

AFISA WA TANAPA AUAWA KWA MSHALE WENYE SUMU, MARA

22 January 2023
Share

Afisa wa TANAPA ameuawa kwa kuchomwa na mshale wenye sumu na wananchi wa Kijiji cha Nyanungu kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara, wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kulinda ndani ya hifadhi ya Serengeti, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro baina ya wananchi na maofisa wa TANAPA ambao wanadaiwa kuwauwa wananchi wanaongia ndani ya hifadhi na kuwanyang'anya mifugo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Meja Jenarali Suleiman Mzee,  kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria mjini Musoma, ambapo amelaani kitendo hicho.