Back to top

DART KUTUMIA MFUMO WA ITS KUSIMAMIA MABASI

20 September 2023
Share

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), umeanza mchakato wa kuandaa mfumo wa utakaorahisisha kusimamia shughuli za upangaji safari za mabasi yaendayo kasi, kulingana na uhitaji wa siku husika pamoja na kutatua changamoto zinazotokea ndani ya mabasi bila wao kuwa kwenye mabasi hayo.
.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede, wakati akiongea na waandishi wa habari, ambapo amebainisha kuwa mfumo huo utasomana na mifumo mingine ambayo tayari ipo ikiwemo ya ukusanyaji fedha.
.
Dkt.Mhede amesema mfumo huo unaojulikana kama Intelligent Transport System (ITS), utapunguza changamoto mbalimbali za uendeshaji mabasi hayo.