
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na oparesheni kali ya kukamata pikipiki na madereva wanaokaidi amri ya kuingia katikati ya jiji.
Jumla ya pikipiki 104 zimekamatwa katika mikoa ya kipolisi Ilala, Temeke na Kinondoni kwa muda wa saa 24 zilizopita.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Sakaam linapiga marufuku madereva wote wanaondesha pikipiki kuingia maeneo ya mjini ikiwa pikipiki hiyo haina kibali cha kuingia maeneo hayo.