Back to top

KAMATI ZA MAAFA MSISUBIRI MAAFA YATOKEE

27 October 2023
Share

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga, amewataka wajumbe wa Kamati za maafa kwenye Wilaya hiyo kutosubiri mpaka maafa yatokee badala yake wanatakiwa waijue historia ya eneo husika, na hatua zitakazorahisisha kujipanga kwa ajili ya maafa yatakayoweza kutokea na kutoa msaada kwa wakati.
.
Ndemanga ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati za maafa kwenye Wilaya hiyo, yaliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa DDC mkoani Lindi, ambapo amebainisha kuwa mafunzo hayo ni moja ya mikakati, ambayo imekuwa ikifanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu katika kupunguza madhara ya maafa kwa kuhakikisha huduma za dharura zinatolewa kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuokoa watu na mali zao.
.
Aidha, Ndemanga amezikumbusha Kamati za Maafa kwenye Wilaya hiyo kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kujiandaa na kukabiliana na maafa pindi yanapotokea.