
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula, amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi nchini, kutumia fursa ya kuruhusiwa mikutano ya hadhara kama njia ya kujibu hoja kwa kuelezea mafanikio ya yaliyofanywa na chama hicho.
Dkt .Mabula amesema hayo, katika ofisi ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza wakati wa mapokezi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa waliochaguliwa hivi karibuni kwenye mkutano mkuu wa 10 wa CCM.
Amesema, wana CCM wasiangalie sasa ambapo mikutano imeruhusiwa na kuanza kubishana huku wakiacha kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuifanya kusuasua.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Chama cha Mapinduzi kinayo matawi, Mashina pamoja na Kamati zake zake za siasa katika ngazi zote na kinachotakiwa ni kurudi kwa wanachama na kuhamasisha maendeleo huku wakikagua utekelezaji wa ilani ya CCM.
Lazima kwenda kila ngazi kwa kukagua na kuangalia kama ilani inatekelezwa lakini siyo kwa kunyanyasa watumishi, hoja ya msingi hatutakiwi kuzifanya hoja zinazokuja kama kero za kujibishana na kila changamoto itakoyokuja igeuzwe kama fursa ya kusonga mbele.
Aidha, amemsifu na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt.Samia Suluhu Hassan na kueleza kuwa kama kuna mtu ambaye watanzania watamkumbuka basi ni yeye kutokana na hekima na busara zake hasa kwa serikali yake ya awamu ya sita kuwa kiungo kizuri cha kuendeleza yale mazuri yote ya serikali ya awamu yaliyopita
Kikubwa anachokifanya kama mama ni hekima, busara na maamuzi yake ni furaha kwa watanzania suala la mariasdhiano lililofanyika ninachotaka kuwaomba wana ccm wenzangu maridhaino ni mchakato, hoja ya msingi hapa tusizifanya hoja zinazoibuliwa katika mikutano kama hoja za kubishana bali ziwe za kutoa majibu kwa yale yaliyofanyika. amesema Dkt Mabula.