Back to top

LAAC: FUATENI TARATIBU ZA MANUNUZI KWENYE MIRADI

23 March 2024
Share

Kamati ya Kudumu ya Bunge za Serikali za Mitaa (LAAC), imeutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, kuhakikisha unafuata sheria, kanuni na taratibu za ununuzi kila unapoanza kutekeleza miradi ya ujenzi kwenye Halmashauri hiyo.
.
Agizo hilo limetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mh. Staslaus Mabula, alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara, ambapo yeye na Kamati yake walibaini kuwa taratibu nyingi za manunuzi kwenye mradi huo, hazikufuatwa ikiwemo ununuzi wa vifaa vya ujenzi kukunuliwa  kwa wazabuni, ambao hawajaidhinishiwa na Wakala la Ununuzi Serikalini (GPSA) pamoja na nukuu za bei kutoidhinishwa na Bodi ya Zabuni ya Halmashauri.
.
Katika hatua nyingine Halmashauri hiyo, imetakiwa kuhakikisha inajibu hoja 10 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2021/22 na kuhakikisha wanawasilisha vielelezo muhimu vinavyohitajika ili kufunga hoja hizo.