Back to top

SEHEMU YA FEDHA ZIELEKEZWE KWENYE LISHE - MOLLEL

23 August 2023
Share

Serikali imesema sehemu ya fedha zilizoletwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia, pamoja na Shirika la Global Financing Facility, kwaajili ya kuboresha mpango wa Uwekezaji Katika Afya ya Mama na Mtoto Tanzania wa miaka mitano (Tanzania Martenal & Child Health Investment Program), zielekezwe kwenye eneo la lishe, katika kipindi cha ujauzito na baada ya mama kujifungua ili kupata watoto wenye uwezo mkubwa kiakili na afya utakaosaidia kuleta maendeleo ya nchi.
.
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt.Godwin Mollel wakati wa uzinduzi wa mpango huo, wenye lengo la kuimarisha afya ya Mama na mtoto nchini, uliozinduliwa na Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman kwa niaba ya Rais wa Zanzibar.