Back to top

Serikali yataifisha madini ya Tanzanite

29 July 2020
Share

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara imetaifisha madini ya Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18 baada ya kumtia hatiani dalali wa Madin Bw.Lucas Kiaseki mkazi wa Mirerani wilayani Simanjiro aliyekutwa na madini hayo baada ya kufanya jaribio la kuyavusha kwenye kizuizi cha lango kuu la mgodi wa madini hayo uliozunguukwa na ukuta.

Akisoma hati ya mashtaka,mkuu wa mashtaka mkoa wa Manyara Bw.Mutalemwa Kisheri mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Bw.Simon Kobelo amesema mshtakiwa Lucas Kisenyi alitenda kosa hilo Aprili 22 mwaka huu baada ya upekuzi kwenye lango la mgodi huo na kukutwa na madini yenye uzito wa gram 132.64 pasipokuwa na leseni ya umiliki wa madini hayo.

Aidha kulingana na mwenendo wa shauri hilo,mshtakiwa huyo aliandika barua kwa mkurugenzi wa mashtaka akiomba kufanya makubaliano ya kukiri kosa hilo na kukubali kulipa fidia kwa serikali.

Kabla ya hakimu Kobelo kuridhia ombi hilo katika shauri hilo no 5 lililokuwa likisikilizwa na mawakili watatu wa upande wa serikali mahakama ndipo iliporidhia  ombi la mshtakiwa na kutoa hukumu ya kulipa asilimia 15 ya shilingi mil 2,706,934/12 inayotokana na gharama ya awali ya malipo ya shilingi mil 18,446,894/10 ya thamani ya madini hayo yaliyokamatwa.

Hata hivyo mawakali wa upande wa serikali ulioongozwa na mkuu wa mashtaka ambae pia ni wakili mwandamizi Bw. Mutalewa uliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu itakayokuwa fundisho mbali na kutaifisha madini hayo na ndipo hakimu Kobelo aliporidhia na kumhukumu mshtakiwa Lucas Kiaseki kutumikia kifungo cha nje cha mwaka mzima akiwa chini ya uangalizi wa kutorudia tena kutenda kosa hilo.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa wakili wa mwandamizi wa serikali Bw.Mutalemwa amesema madini hayo yametaifishwa na kupelekwa benki kuu kulingana na sheria inavyotaka.