Back to top

WAKULIMA SONGEA WAKABIDHIWA HATIMILIKI ZA MASHAMBA

20 December 2018
Share

Serikali kwa kushirikiana mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania MVIWATA mkoani Ruvuma imetoa hatimiliki za mashamba kwa wakulima 557 wa vijiji vinne wilayani Songea ni katika hatua ya kurasimisha maeneo hayo pamoja na kusuluhisha migogoro ya ardhi.

Hayo yamebainishwa na afisa mwandamizi wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania MVIWATA mkoani ruvuma bi. Laika Nasoro wakati akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi hatimiliki za kimila za mashamba 220 kwa wakulima wa kijiji cha Lusonga ambacho ni miongoni mwa vijiji vinne vilivyonufaika na hati hizo.

Kwa upande wao wakulima wa vijiji hivyo wanasema kuwa hati hizo za ardhi zitasaidia kuondoa migogoro ya ardhi iliyokuwa ikijitokeza mara kwa mara miongoni mwao na kwamba hati hizo zitawasaidia wao kujikwamua kiuchumi kwa kuzitumia katika dhamana ya kuombea mikop katika tyaasisi mbalimbali za kifedha..