Back to top

Watahiniwa 333 wafutiwa matokeo kwa udanganyifu katika mtihani.

09 January 2020
Share

Baraza la mitihani Tanzania latangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na maarifa QT, kidato cha pili  na darasa la nne ambayo iliyofanyika mwezi Novemba mwaka jana,huku hilo  likifuta matokeo yote ya watahiniwa 333 waliofanya udanganyifu katika mtihani .

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji NECTA Charles Msonde amesema Watahiniwa 340,914 ndio wamefaulu mtihani wa kidato cha nne , Kati ya watahiniwa 422,722 waliofanya mtihani huku wasichana waliofaulu wakiwa ni 175,296 sawa na asilimia 79.46 na wavulana 165,681 sawa na asilimia 81.94.

Takwimu za matokeo zinaonesha kuwa watahiniwa wamefanya vizuri zaidi katika masomo mengi ya msingi ambapo ufaulu wa masomo hayo Uko juu wastani kati ya asilimia 51.25 na 91.31, huku watahiniwa wakishindwa kufanya vizuri katika masomo ya mawili ya physics na basic mathematics yakionekana.