
Wagonjwa wawili waliokuwa wanaumwa na ugonjwa Corona wamefariki nchini Tanzania leo na kufanya idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kufikia watatu.
Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu amethibisha, huku akisema waliofariki ni wanaume, mmoja ana miaka 51 na mwingine 57 na wote ni Watanzania wakazi wa Dar es Salaam.
Waziri Ummy ameeleza kuwa wagonjwa waliothibishwa kupata maambukizi ya virusi vya Corona nchini ni 32, idadi hiyo imeongezeka baada ya leo Aprili 10, 2020 Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutangaza uwepo wa wagonjwa wapya wa wili wa Corona visiwani humo.
Kwenye Taarifa yake Waziri Ummy ameeleza kuwa kati ya watu hao tano wamepona na wagonjwa wengine 24 wanaendelea na Matibabu, ambapo ameendelea kuwasisitiza wananchi kuendelea kuchukua Tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Tazama Jedwali hapo kama linavyojieleza.