Matumaini ya mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, yameanza kurejea baada ya kifungo chake cha miaka minne kwa kosa la kutumia dawa za kusisimua misuli kupunguzwa hadi miezi 18, kufuatia rufaa iliyofanikiwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (Cas).