Kamati ya Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ikiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Mhe. Dkt. Emanuel Qambaji Nuwas, na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Yeconia Deles, wametembelea banda la Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Jijini Dar es Salaam.










